Jeshi la Ethiopia na wapiganaji wa Tigray wajizatiti kusitisha mapigano

Katika juhudi za kusitisha machafuko yanayoghubika nchi ya Ethiopia, serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Tigray wanajizatiti kuhakikisha ghasia hizo ambazo zimedumu kwa muda wa miezi 14, zinasitishwa na kurejelewa kwa hali ya amani.

Kulingana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, juhudi muafaka za kuleta amani nchini Ethiopia zimeanzishwa baada ya mwaka mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Also Read
Wafalme wa soka Al Ahly wapigwa na butwaa nyumbani na Masandawana

Guterres alisema hayo baada ya kukutana na mjumbe wa eneo la upembe wa Afrika wa Muungano wa Afrika Olusegun Obasanjo, aliyemfahamisha kuhusu juhudi hizo.

“Ninafuraha kwamba baada ya mwaka mmoja wa mapigano ambayo yamewaathiri mamilioni ya watu nchini Ethiopia na katika kanda hiyo, sasa ni wazi kwamba kuna juhudi za kuleta amani,” alisema Guterres.

Also Read
Uhuru Kenyatta: Kenya imejitolea kukuza demokrasia

Obasanjo amekuwa akikutana na maafisa wa serikali ya nchi ya Ethiopia na kundi la wapiganaji la Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Obasanjo alisema muungano wa Afrika una matumaini kwamba sasa kuna nafasi ya kutatua mizozo ya kisiasa na kidoplamisa.

Kulingana na Guterres, Umoja wa Mataifa utaunga mkono mchakato wa kuleta amani nchini Ethiopia ambao unajumuisha pande zote.

Also Read
Jaji Mkuu Martha Koome afanya mabadiliko katika Mahakama ya ajira na maswala ya leba

Vikosi vya kijeshi vimekuwa vikikabiliana na waasi Kaskazini mwa nchi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja ambapo zaidi ya maelfu ya watu wamefariki.

Mjumbe wa Marekani wa upembe wa Afrika David Shatterfield na naibu waziri wa maswala ya Afrika Molly Phee, wanatarajiwa kuzuru Ethiopia baadaye wiki hii.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Kenya kukabana koo na Puerto Rico mechi ya mwisho ya kundi A mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi