Jeshi la Uganda latoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la mapinduzi

Mwana wa kiume wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kwamba haitachukua hata siku moja kwa jeshi la nchi hiyo kuzima jaribio lolote la mapinduzi, jinsi ilivyofanyika nchini Guinea ambako Rais Alpha Condé aling’olewa mamlakani.

Luteni Generali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ndiye kamanda wa majeshi ya nchi kavu, alisema kupitia kitandaazi cha tweeter  kwamba mwanajeshi yeyote akijaribu kujihusisha na maasi ataadhibiwa vikali.

Also Read
Rwanda Uganda waumiza nyasi bila lengo

Katika ujumbe huo alijumuishsa picha ya kanali Mamadu Doumbouya, afisa aliyeongoza mapinduzi nchini Guinea.

Juma lililopita, Museveni aliwataka viongozi wa mapinduzi nchini Guinea kuondoka, akisema kung’atuliwa kwa Rais wa taifa hilo ni hatua inayorudisha nyuma maendeleo.

Also Read
Rais Kenyatta amuomboleza mbunge wa zamani wa Kamukunji George Nthenge

Condé – ambaye ameiongoza Guinea kwa mihula mitatu – aling’atuliwa uongozini tarehe 5 Septemba mwaka 2021 na kikosi kikosi maaalum cha wanajeshi.

Wanajeshi hao walimshtumu kwa usimamizi mbaya na pia ufisadi. Mapinduzi hayo yameshtumiwa na viongozi mbali mbali nje ya taifa hilo la Afrika Magharibi, lakini raia wengi wa Guinea wameunga mkono kuondolewa mamlakani kwa Rais huyo mwenye umri wa miaka 83, huku wakihimiza jeshi kuharakisha mipango ya kurejesha utawala mikononi mwa raia.

Also Read
Malkia Strikers kufungua Olimpiki dhidi ya wenyeji Japan Jumapili adhuhuri

Mapinduzi hayo yalisababisha taifa hilo kuondolewa katika yanachama wa tume ya muungano wa Afrika sawia na Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi