Gavana wa jimbo la Texas nchini Marekani Greg Abbott ametangaza kuwa jimbo hilo litaondoa agizo la watu kuvaa barakoa kwenye maeneo ya umma na kuruhusu biashara kufunguliwa mnamo wiki ijayo.
Jimbo la Texas ndilo kubwa zaidi nchini Marekani kuondoa agizo la watu kuvaa barakoa kwenye maeneo ya umma.
Abbott amekosolewa na chama chake kuhusiana na hatua hiyo, ambayo ilianza kutekelezwa mwezi Julai mwaka uliopita.
Lakini utawala wa Joe Biden umesisitiza kuwa vizuizi vya kukabiliana na maradhi ya COVID-19 vingali muhimu.
Tangazo hilo limetolewa huku masharti kama hayo yakiondolewa katika majimbo mengine ikiwemo Michigan, Louisiana na Mississippi ambayo pia yameondoa maagizo ya kuvalia barakoa.
Utoaji wa chanjo za kukabiliana na virusi vya korona umetoa matumaini ya watu kurejelea maisha ya kawaida nchini Marekani.
Rais Joe Biden amesema kuwa taifa hilo lina chanjo za kutosha watu wazima wote katika taifa hilo kufikia mwezi Mei.
Hatua ya majimbo kuondoa masharti ya kukabiliana na maradhi ya COVID-19 ni kinyume na utawala wa Biden na wataalam wake wakuu wa afya ambao wamesikitishwa na hatua hizo huku janga hilo likibakia kuwa tisho.