Joash Onyango Akubali Mkataba Mpya na Simba SC

Taarifa kutoka klabu ya mchezo wa soka ya Simba SC nchini Tanzania zinaashiria kwamba beki wao Joash Onyango mzaliwa wa Kenya, amekubali kutia saini mkataba kwenye timu hiyo huku mkataba wa sasa ukitarajiwa kutamatika mwisho wa mwezi Julai mwaka 2022.

Joash Onyango anasemekana kukubali mkataba mwingine wa miaka miwili baada ya taarifa za awali kuashiria kwamba alikuwa akiviziwa na timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Mwezi Januari mwaka huu wa 2022 iliripotiwa kwamba Onyango ambaye alijiunga na Simba SC almaarufu wekundu wa msimbazi mwaka 2020 mwezi Julai kutoka Gor Mahia ya Kenya alikuwa ametoa matakwa ambayo alitaka yatimizwe na Simba SC ili akubali mkataba mpya.

Also Read
Harambee Stars yafungua Kambi ya mazoezi kujiandaa kuikabili Misri Alhamisi
Also Read
Pompeo: Afisa wa ngazi ya juu Urusi aliamuru Navalny apewe sumu

Matakwa ya Onyango ni pamoja na malipo yake ya usajili ya shilingi milioni 5 za Kenya na mshahara wa kila mwezi wa shilingi laki tano unusu za Kenya. Haijulikani ikiwa Simba SC iliridhia matakwa yake ndiposa akakubali kutia saini mkataba mpya.

Onyango wa umri wa miaka 29 alianza kucheza soka ya kulipwa kwenye kilabu ya West Kenya Sugar FC ambayo haiko kwa sasa, kisha akajiunga na Western Stima ambayo pia haipo sasa. Aliafikia ufanisi kama mchezaji alipojiunga na Gor Mahia mwezi Januari mwaka 2017. Baadaye alianza kuichezea timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars kabla ya kujiunga na wekundu wa msimbazi nchini Tanzania.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Watu 171 wafariki kwenye mkanyagano wakati wa mechi ya soka nchini Indonesia

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi