Joeboy awasili Tanzania

Msanii wa muziki toka nchini Nigeria Joseph Akinwale Akinfenwa-Donus maarufu kama Joeboy amewasili Tanzania ambapo alilakiwa na mwenyeji wake mwanamuziki Nandy. Joeboy ndiye msanii mkubwa kutoka nje ya Tanzania ambaye atatumbuiza kwenye Nandy Festival awamu ya mji wa Arusha.

Wasanii wengine ambao wamealikwa kutumbuiza kwenye Nandy Festival Arusha katika eneo la Eden Garden ni Masauti na Tanasha Donna kutoka Kenya, Professor Jay, Kundi la Weusi, Mabantu, Nally, Adam Mchomvu na Mr Blue kati ya wengine wengi.

Also Read
Gigy Kafunguliwa!

Mchekeshaji wa Kenya Jalang’o naye yuko kwenye mabango ya walioalikwa kutumbuiza kwenye Nandy Festival Arusha kesho Jumamosi tarehe 10 mwezi Julai mwaka 2021 kuanzia saa moja jioni.

Also Read
Studio za Eric Omondi zafungwa

Tamasha la Nandy Festival lilizinduliwa rasmi tarehe 11 mwezi Mei kwenye kikao na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam na kwenye kikao hicho Nandy alitangaza kwamba sehemu ya kwanza kupeleka burudani ni Kigoma.

Awamu ya Kigoma ilifanyika tarehe 5 mwezi Juni mwaka huu wa 2021 katika uwanja wa michezo wa Mwanga Center. Tarehe 19 mwezi wa sita Nandy Festival ilifanyika Mwanza, tarehe 26 mwezi wa 6 ikafanyika Dodoma na sasa ni zamu ya Arusha.

Also Read
Emmanuel Ehumadu ashutumiwa kwa kukusanya pesa za mazishi ya Asuzu

Nandy festival inadhaminiwa kwa kiasi kikubwa na Tanzania Telecommunications Corporation ambayo ni kampuni ya mawasiliano inayomilikiwa na serikali na ndio maana inaitwa “TTCL Nandy festival”.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi