John Mahama ajiondoa kuwa mjumbe maalum nchini Somalia

Aliyekuwa Rais wa Ghana, John Mahama amejiondoa kwenye uteuzi wa mjumbe maalum wa Muungano wa Afrika wa kuongoza mazungumzo ya kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Somalia.

Mahama alitaja kutojitolea kwa serikali za majimbo nchini Somalia kuwa sababu ya kujiondoa kwake.

Also Read
Jamii ya kimataifa yatakiwa kuangazia habari njema kutoka Afrika

Muungano wa ulaya ulimteua Mahama kuwa mjumbe maalum nchini Somalia mapema mwezi Mei, lakini taifa hilo lilimkataa kwa madai kwamba alikuwa na upendeleo.

Somalia inamshutumu Mahama kwa kuwa na uhusiano wa karibu na Kenya, ikikariri kwamba mjumbe huyo anapaswa kuwa mtu asiyeegemea upande wowote.

Also Read
Rais mpya wa Marekani Joe Biden aanza kazi rasmi kwa mageuzi ya sheria

Kenya na Somalia zimetofautiana kidiplomasia huku Somalia ikiishutumu Kenya kwa kuingilia kati masuala ya taifa hilo, madai ambayo Kenya imekanusha.

Also Read
Kenya yarejesha uhusiano wa kidiplomasia na Somalia

Uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Kenya na Somalia uko katika hali ya ati ati. Awali mataifa haya mawili yalifunga uhusiano wao wa kidiplomasia kabla ya kurejesha kupitia juhudi za Qatar.

  

Latest posts

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Kero la utekaji nyara lahofisha wanafunzi kurejea shuleni Nigeria

Tom Mathinji

Zimbabwe: Watumishi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya COVID-19 waadhibiwa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi