Jonathan Mckinstry ateuliwa kocha mpya wa Gor Mahia

Klabu ya Gor Mahia imemzindua Jonathan Mckinstry kuwa kocha mpya kwa mkataba wa miaka 2 ,akijukumiwa kunyakua taji ya ligi kuu.

Kabla ya uteuzi wake Mckinstry amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda Cranes baina ya mwaka 2019-2021, akiwasaidia kunyakua taji ya CECAFA .

Also Read
Rwanda na Tanzania kuandaa mechi za Cecafa kufuzu kombe la Afcon kwa chipukizi
MCkinstry-signing

Pia amehudumu katika wadhfa wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda kati ya mwaka 2015 na 2016 na pia timu ya Siera Leone kati ya mwaka 2013-2014.

Also Read
Carlos Manuel Vaz Pinto ateuliwa kocha mpya wa Gor Mahia

Mwingereza huyo pia amekuwa usukani katika klabu ya Saif Sporting Club,katika ligi kuu nchini Bangladesh Premier League kati ya mwaka 2018-2019 na FK Kauno Zalgiris katika ligi kuu ya Lithuania kutokea mwaka 2017 na 2018.

Also Read
Kocha mpya wa Gor Mahia Vaz Pinto asaini mkataba wa miaka miwili

Kogalo wataanza harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu tarehe 27 mwezi ujao,baada ya kukosa taji hiyo kwa misimu miwili mtawalia.

  

Latest posts

Brigid Kosgei ajiondoa London Marathon kutokana na jeraha

Dismas Otuke

Malkia Strikers yasaka ushindi wa kwanza dhidi ya Cameroon mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Gavana wa Mombasa Abdulswamad atangaza mabadiliko ya usimamizi wa kaunti

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi