Jopo labuniwa kutatua changamoto katika mbuga ya kitaifa ya Nairobi

Serikali imebuni jopo maalum la kushughulikia changamoto zinazokumba mbuga ya kitaifa ya Nairobi.

Jopo hilo  litaongozwa na  Dr. Helen Gichohi.

Waziri wa utalii  Najib Balala amesema kuwa jopo hilo linatarajiwa kuwasilisha ripoti yake katika muda wa miezi mitatu.

Also Read
Naomi Campbell sasa ni mzazi

Jopo hilo linatarajiwa kuorodhesha mahala ambapo barabara  itajengwa ili kuruhusu wanyama pori kuhama kwa urahisi kutoka mbuga ya taifa ya Nairobi hadi katika eneo la Swara-Kapiti plains.

Also Read
Balala: Ushirikiano wa sekta ya uchukuzi wa angani utabuni nafasi zaidi za ajira Afrika

Wakati wa uzinduzi wa jopo hilo, Balala alilitaja  wakati huo kuwa wa kihistoria ambao utashuhudia mbuga hiyo ikiongeza upana kutoka ekari elfu 29 hadi ekari elfu 78.

Mbunga hiyo ya kitaifa ya Nairobi ambayo inajivunia kuwa mbuga ya kipekee ya wanyama iliyo katika mji mkuu ulimwenguni, imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na maswala ya miundo misingi na maendeleo ya binadamu.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi