Juhudi za kimataifa zaanzishwa kuipiga jeki India inayopambana na wimbi kali la korona

Juhudi za kimataifa zimeanzishwa ili kuisaidi India, ambayo imekumbwa na uhaba mkubwa wa hewa ya oksijeni inapopambana na msambao mbaya zaidi wa ugonjwa wa COVID-19.

Uingereza imepeleka vifaa vya kusaidia kupumua na vifaa vya hewa ya oksijeni, huku shehena ya kwanza ikitarajiwa kufika nchini India hapo kesho.

Aidha mataifa ya Muungano wa Ulaya yameahidi kupeleka misaada yao kwa nchi hiyo kwa kuzingatia  kipengee katika sheria zake cha ulinzi wa raia.

Also Read
Hakuna maafa yaliyotokana na COVID-19 Kenya kwa siku ya pili mfululizo

Rais wa Jumuiya ya Ulaya Ursula von der Leyen aliandika ujumbe wa Twitter, akisema kuwa kamati kuu ya jumuiya hiyo tayari inashauriana na mataifa wanachama, ambayo yako tayari kusaidia kwa hewa ya oksijeni na dawa.

Kutokana na hali hiyo ya dharura, Marekani imeondoa marufuku ya kupeleka nje mali ghafi, ili kuiwezesha India kutengeneza shehena zaidi ya chanjo aina ya AstraZeneca.

Also Read
Trump aonywa dhidi ya kutumbukia mtegoni kuhusu madai ya vita kati ya Marekani na Israeli

Mji mkuu wa India New Delhi umeongeza muda wa kusitisha shughuli, huku hospitali ambazo zimefurika wagonjwa, zikiwaambia baadhi ya wagonjwa kuwa hazina uwezo wa kuwahudumia.

Serikali ya India imeidhinisha viwanda 500 vya kutengeneza hewa ya oksijeni nchini humo kuimarisha uzalishaji wa hewa hiyo.

Also Read
Raia wa Brazil waandamana dhidi ya Rais Jair Bolsonaro kwa ushughulikiaji duni wa janga la COVID-19

India imeripoti takriban visa 349,691 vipya vya ugonjwa wa COVID -19 katika muda wa saa 24 na vifo vya watu 2,767 katika kipindi hicho. Hata hivho idadi halisi inadhaniwa kuwa ya juu kuliko hiyo iliotolewa.

Wakati uo huo, Banglaesh imetangaza kwamba itafunga mipaka yake na India kuanzia leo ili kuzuia msambao wa ugonjwa huo.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi