Juhudi za miaka 100 za CPC zina maana gani kwa nchi za Afrika?

Na Hassan Zhou – CMG.

Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimekuwa madarakani kwa miaka sabini na mbili. Kupitia uongozi wake, China imeinuka na kuwa nchi ya pili yenye uchumi mkubwa duniani.Kikao cha 6 cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 19 ya CPC kilichomalizika hivi karibuni, kimejumuisha jinsi chama hicho kilivyoiongoza China kupata maendeleo ya uchumi na utulivu wa jamii.

Hizi ni juhudi ambazo zina maana kubwa hasa kwa nchi za Afrika. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania Profesa Humphrey Moshi aliandika makala kwenye gazeti la The Guardian la nchi hiyo, kuwa CPC siku zote inaunga mkono utaratibu wa pande nyingi, kuchukulia “usawa na udhati” kama msingi wa uhusiano kati ya China na Afrika, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana na nchi za Afrika.

Mwezi Aprili mwaka 1955, mkutano wa Bandung wenye maana ya kihistoria ulifanyika. Kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zilizotolewa na hayati waziri mkuu wa China Zhou Enlai zilifungua ushirikiano wa nchi za Kusini na uhusiano wa kisasa kati ya China na Afrika.

Also Read
Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Baada ya mkutano huo, China na Afrika zilianza kujenga uhusiano wa kiwenzi wa aina mpya. CPC iliziunga mkono sana nchi za Afrika kupambana na ukoloni na kutafuta maendeleo ya kujitegemea, huku vyama mbalimbali vya kisiasa vya Afrika vikijifunza uzoefu na maarifa muhimu kutoka kwa China.

Tayari ushirikiano kati ya China na Afrika ulikuwa umepata maendeleo, na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC lililozinduliwa mwaka 2000 liliinua uhusiano kati ya pande hizo mbili hadi kwenye kiwango cha juu zaidi, cha sekta nyingi zaidi na cha kimkakati zaidi.

Katika miaka 20 iliyopita, China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika, na mwaka 2019 thamani ya biashara kati yao ilifikia dola za kimarekani bilioni 208.

China imejihusisha kwenye sekta mbalimbali za ujenzi wa miundombinu barani Afrika, na kutoa msaada mkubwa katika mambo ya usafiri, mawasiliano ya simu, maji safi, nishati n.k. Katika kupambana na janga la COVID-19 ambalo limewaua watu zaidi ya milioni 5 duniani, China pia imetoa msaada mwingi kwa Afrika.

Also Read
Watu 30 watekwa nyara nchini Nigeria

Lakini kwa nchi za Afrika, nafasi ya China sio tu ni mwenzi wa kidiplomasia au nchi inayotoa msaada wa kiuchumi, bali pia maendeleo yake yana maana kwa nchi za Afrika.

Moja ya maana hizi ni kushikilia uongozi wa CPC na kutoa kipaumbele kwa maslahi ya watu. Mfumo wa kidemokrasia mashinani umehakikisha kuwa watu wana haki za kutoa maoni juu ya masuala yanayohusu maisha yao, huku utaratibu wa kuchagua watu mashuhuri wa ngazi ya juu unahakikisha watu wenye vipaji vya uchumi, sayansi na uhusiano wa kimataifa wanaongoza nchi na kutoa maamuzi sahihi katika kutunga sera za taifa.

Cha muhimu zaidi ni kuwa hii inahakikisha siasa na sera zinakuwa endelevu, jambo ambalo ni muhimu kwa nchi za Afrika. Pili, kama CPC, katika kuongoza nchi kutunga sera za kiuchumi na kijamii, nchi za Afrika zinapaswa kufanya uvumbuzi kwa nadharia zilizopo, kutoa maamuzi kwa kujitegemea na kufuata njia ya taifa lenyewe.

Also Read
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Algeria na Ufaransa wadorora

Ingawa China imejifunza uzoefu na mitindo ya nchi za nje katika kujiendeleza, lakini sio kama inaiga moja kwa moja, bali inatunga sera zake kwa mujibu wa historia, utamaduni, jiografia na siasa.

Aidha, CPC inashikilia kujifanyia mapinduzi, kwa mfano China imeshughulikia vizuri suala la ufisadi, ambalo bado ni tatizo sugu linalokwamisha maendeleo ya Afrika.

Mapema karne ya 20, CPC ikiwa ni chama kidogo chenye wanachama wapatao 50 kilianza safari yake ya miaka 100 ya kwanza, sasa kinaingia kwenye miaka 100 ya pili na kuongoza nchi inayowajibika na kujenga dunia.

Katika siku za baadaye, CPC inatarajiwa kushirikiana na nchi nyingine na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Marekani kutatua mzozo wa mpakani baina ya Israel na Lebanon

Tom Mathinji

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Burkina Faso Paul-Henri Damiba ajiuzulu

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi