Juma Nature ateuliwa balozi wa Temeke

Msanii wa muda mrefu wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Juma Nature ameteuliwa kuwa balozi wa eneo la Temeke.

Meya wa eneo hilo Abdalla Mtinika ndiye alitangaza uteuzi wa Nature kama balozi wakati anaendeleza harakati za kuteua watu maarufu kama mabalozi wa eneo hilo.

Juma Nature sasa anajiunga na wengine kama vile mchekeshaji Eric Omondi wa Kenya na mcheza soka wa asili ya Tanzania Mbwana Samatta kwenye wadhifa huo wa ubalozi wa Temeke.

Also Read
Roma Zimbabwe kuacha kazi ya muziki

Meya Mtinika alisema kwamba ni fursa haikuwa imejitokeza ya Juma Nature kufika afisini kukabidhiwa bendera rasmi lakini yeye alikuwa tayari balozi.

Nature anatarajiwa kutumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba Temeke imekuwa na mazingira safi, ulinzi na asaidie kwenye kampeni dhidi ya mihadarati.

Also Read
Kapedo Aelezea alivyoathirika na Janga La Corona

Eric Omondi alipotangazwa kuwa balozi wa Temeke malalamiliko yalisheheni vinywa vya watanzania hasa wasanii ambao hawakuelewa jinsi mtu wa nje alitambuliwa nyumbani kwao ilhali Kuna nyota wengi wanaostahili kazi hiyo.

Juma Kassim Ally maarufu kama Juma Nature ambaye sikuhizi anajiita Sir Nature alianza muziki mwaka 1998 na ni mwanzilishi na mmoja wa wanamuziki wa Kundi la TMK Wanaume.

Also Read
Filamu kupelekwa mashinani

Yeye hutumia nyimbo zake kuendeleza uanaharakati wa maswala kadhaa ya kijamii kama vile janga la Ukimwi Kati ya mengine.

Amewahi kuteuliwa kuwania tuzo za Tanzania Music Awards mwaka 2005 katika kitengo cha albamu bora ya hip hop kwa kazi yake iitwayo “Ubinadamu Kazi”.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi