Junet aomba msamaha kwa kumdhalilisha Seneta Mwaura kwa misingi ya ulemavu

Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed ameomba msamaha kwa jamii ya watu wanaoishi na ulemavu kufuatia matamshi yake yaliyoonekana kumdhalilisha Seneta Maalum Issac Mwaura.

Kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Junet hata hivyo amefafanua kuwa matamshi yake hayakulenga kuwadhalilisha watu wanaoishi na ulemavu huo bali alikuwa amedhamiria kumshtumu Mwaura ambaye amedai anatumia hali yake kujinufausha kisiasa.

Mbunge huyo alinukuliwa akisema kuwa Seneta Mwaura hutumia ujanja wa kujibadilisha rangi ya ngozi ili aonekani kuwa ni mlemavu na kuteuliwa bungeni kuwakilisha walemavu.

Also Read
NCIC yatoa ilani kwa wachochezi wa uhasama miongoni mwa jamii za Marsabit
Also Read
Huenda bara Afrika likapoteza asilimia 30 ya pato jumla kutokana na mabadiliko ya hali ya anga

Matamshi hayo yaliwakasirisha watu wanaoishi na ulemavu, ambao wameitisha kikao na waandishi wa habari na kumkosoa mbunge huyo, wakisema matamshi hayo ni ya kudhalilisha na pia yanaibua uchochezi dhidi ya walemavu.

Haya yanajiri huku Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) ikilenga kumchukulia hatua Junet kwa matamshi aliyotoa dhidi ya Seneta Mwaura.

Also Read
NCIC yataka mamlaka zaidi kukabiliana na matamshi ya chuki

Tume hiyo imesema kwamba inachunguza swala hilo kwa nia ya kuchukua hatua zinazofaa.

Matamshi ya Junet pia yamelaaniwa na Wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambao wanasema alikosea kutumia rangi ya ngozi ya Mwaura kwa masilahi yake ya kisiasa.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi