Justin Muturi: EACC ilijaribu kuhujumu safari yangu ya Ikulu

Spika wa bunge la taifa, Justin Muturi, amefichua kwamba tume ya maadili na kupambana na ufisadi hapa nchini EACC, ilijaribu kumhangaisha na masuala bandia baada ya kutangaza azma yake ya kuwania urais.

Akiongea nyumbani kwake huko Kanyuambora, Mbeere-kaskazini wakati wa mkutano na viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya mashariki, Muturi alisema viongozi hawapaswi kuhangaishwa kwa sababu ya miegemeo yao ya kisiasa.

Also Read
Tabasamu kwa wakazi wa Naisoya, Kaunti ya Narok, baada ya serikali kuwapa hati miliki za ardhi

Muturi alisema azma yake ya kuwania urais inazingatia kuleta uadilifu na utangamano humu nchini. Spika Muturi alisema hivi karibuni atazindua chama chake cha kisiasa ambacho atakitumia kuwania urais.

Kulingana na Spika huyo, wakati huu eneo la Mlima Kenya mashariki hautatumika tena kuwasaidia watu wengine bila kunufaisha eneo hilo.

Also Read
Waiguru: EACC inatumiwa kunihujumu kisiasa

“Bunge lijalo litaapishwa mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka 2022, huo ndio wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta atakabidhi mamlaka kwa atakaye mridhi. Mnaona nyinyi atapea nani,” aliuliza Muturi.

Also Read
Prof. Magoha: Asilimia 80 ya wanafunzi wamerejea shuleni

Viongozi hao kutoka mlima Kenya mashariki walitoa wito kwa Muturi kutangaza chama chake cha kisiasa haraka iwezekanavyo. Viongozi hao waliotoka katika kaunti za Tharaka Nithi, Meru na Embu walisema ni wakati wa eneo la Mlima Kenya mashariki kutoa Rais wa tano wa taifa hili.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi