Kaburi La Pop Smoke Lavunjwa

Maafisa wa polisi huko New York nchini Marekani wanachunguza kisa cha kaburi la mwanamuziki Bashar Barakah Jackson maarufu kama Pop Smoke kuvunjwa mwishoni mwa Juma lililopita.

Waliovamia kaburi hilo wanasemekana kujaribu kuburuta jeneza lake Jumamosi baada ya kuvunja ukuta wa kaburi hilo ambao ulikuwa na jina la marehemu.

Also Read
Brandy kurejelea uigizaji

Picha ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni zinaonyesha vifusi vilivyotokana na ubomozi wa kaburi hilo katika makafani ya Green-Wood.

Msemaji wa eneo hilo la makaburi Jeff Simons, alielezea wanahabari kwamba waligundua uvamizi huo na mara moja wakafahamisha polisi na familia ya marehemu.

Also Read
Ragga Dee apuuza Bobi Wine

Simons hakutoa maelezo zaidi na haijulikani ikiwa wavamizi walifanikiwa kutoa jeneza hilo.

Pop Smoke, aliuawa mwezi Februari mwaka jana akiwa na umri wa miaka 20, na watu watano ambao walimvamia nyumbani kwake.

Also Read
Anderson .Paak atoa onyo

Kifo chake kilijiri siku 12 tu baada ya kuzindua albamu yake wakati wengi waliamini kwamba angefanya vyema katika ulingo wa muziki siku zijazo.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi