Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ametangaza rasmi kuwa amejiondoa kutoka chama cha muungano wa Azimio la Umoja,One Kenya.
Kulingana na Kalonzo, Vyama vingine tanzu vya muungano wa One Kenya ambavyo vilikuwa vimejiunga na chama hicho cha muungano pia vimejiondoa.
Makamu huyo wa Rais wa zamani alithibitisha kwamba, muungano wa One Kenya alliance umerejeshwa, huku akitangaza kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe tisa Agosti mwaka huu.
Kalonzo atawania wadhifa wa Urais akiwa na mgombea mwenza Andrew Leteipa Sunkuli.
Kalonzo amesema Sunkuli ni mwanasiasa aliyepanda ngazi kutoka tabaka la chini na ana sifa ya uadilifu na maongozi mema.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu, Kalozo alisema alimchagua Leteipa Sunkuli ili kutimiza makataa ya tume ya uchaguzi ya IEBC.
Kalonzo alisema hajuti kuchukua hatua hiyo ya mwisho, kwani ilikuwa bayana kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua alipendelewa na Raila Odinga kwa wadhifa huo.
Kalonzo alitumai kuwa angepewa wadhifa wa mgombea mwenza, lakini akapigwa kumbo na waziri huyo wa zamani wa sheria.