Kamala Harris aongoza watu wengine mashuhuri kumkumbuka George Floyd

Mwania mwenza wa Joe Biden kwenye kinyanganyiro cha Urais wa nchi ya Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic Bi. Kamala Harris aliongoza watu wengine mashuhuri katika kumkumbuka marehemu George Floyd kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Jumatano tarehe kumi na nne mwezo Oktoba mwaka 2020 Marehemu George Floyd angeadhimisha miaka 47 tangu kuzaliwa kwake.

Kamala Harris aliandika haya kwenye twitter,

“Leo ingekuwa siku ya kuzaliwa ya 47 ya kusherehekea kuzaliwa kwa marehemu George Floyd. Angekuwa hai hadi sasa kusherehekea siku hii na jamaa na marafiki. Tunahitaji haki itendeke na tuhakikishe hili halifanyiki tena – kuanzia kupiga marufufuku kubanwa koo kwa washukiwa na kuleta kiwango kinachokubalika cha nguvu zitakazotumiwa na polisi dhidi ya washukiwa. ”

Also Read
Trump aondoka katika Ikulu ya Marekani

Watu wengine mashuhuri ambao walimkumbuka marehemu Floyd ni mwanamuziki Beyonce ambaye aliweka picha ya kitambo ya marehemu Floyd akiwa anasoma na kuandika “Siku njema ya kuzaliwa ya milele George Floyd.”

Also Read
Kazi mpya kutoka kwa Mheshimiwa Professor Jay.

Wengine ni Tracee Ellis Ross ambaye ni muigizaji na muimbaji nchini marekani, Amy Schumer mchekeshaji na muigizaji, Martin Luther King III mtetezi wa haki za binadamu na Kerry Washington muigizaji nchini marekani kati ya wengine wengi.

Kerry Washington alihimiza wamarekani wajitokeze kupiga kura kwa ajili ya marehemu George Floyd.

George Floyd ni mmarekani mweusi ambaye aliuawa na polisi nchini marekani mnamo mwezi mei mwaka huu wa 2020 kwa kushukiwa kwa kosa la kulipia bidhaa na noti bandia.

Also Read
Naomi Campbell azuru Kenya

Kwenye video ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, polisi mmoja anaonekana kumbana koo marehemu Floyd kwa kuwekelea goti kwenye shingo akiwa chini na anasikika akisema hawezi kupumua.

Kifo chake kilizua maandamano kote nchini Marekani na hata katika sehemu kadhaa ulimwenguni kwa nia ya kuhimiza kuheshimiwa kwa maisha ya watu weusi.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi