Kamati ya bunge la Seneti yaridhishwa na ustawishaji wa kituo cha Konza

Kamati ya bunge la Seneti kuhusu habari, mawasiliano na teknolojia, imepongeza hatua ambazo zimepigwa katika ustawishaji wa kituo cha teknolojia cha Konza.

Akiongea baada ya kuzuru mradi huo, mwenyekiti wa kamati hiyo aliyepia Seneta wa kaunti ya Baringo Gideon Moi, alisema kamati hiyo imeridhishwa na hatua ambazo zimepigwa katika ustawishaji wa kituo hicho licha ya matatizo ya kifedha.

Also Read
Sisi ndio kusema, EACC yaonya kuhusu maadili ya wanaotaka kuwania nyadhifa serikalini

“Tumefurahishwa na kile wanachofanya,na pia kilichoafikiwa na usimamizi Licha ya kuwa na changamoto za kifedha. Lakini zaidi ya yote tumetiwa moyo kwa kuwa wametimiza lengo lao ambalo walitaka kuafikia Licha ya changamoto,” alisema Seneta Moi.

Also Read
Wakenya wataka kurejeshewa akiba yao ya NSSF

Seneta Moi alikariri kwamba wasimamizi wa kituo hicho wamekibadili kuwa cha ubunifu wa teknolojia sambamba na ruwaza ya maendeleo ya mwaka 2030.

Wakati wa ziara hiyo kamati hiyo ilikagua miradi mbali mbali ikiwa ni pamoja na utenda kazi wa kituo cha kitaifa cha kuhifadhi takwimu kilichozinduliwa mwezi uliopita na Rais Uhuru Kenyatta alipozuru mradi huo.

Also Read
BBI yapata pigo la kwanza Baringo

Wanachama wa kamati hiyo walielezwa kuhusu sekta mbali mbali za mradi huo na hali ya kisheria na kifedha ya kituo hicho cha Konza.maseneta hao walisema wataunga mkono mswada wa Konza ili kituo hicho kitambuliwe kisheria.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi