Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Kamati kuu ya kusaidia rais mteule kuchukua hatamu za uongozi imeandaa kikao cha kwanza kabisa na wanahabari. Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mkuu wa utumishi wa umma Bwana Joseph Kinyua alisema kwamba aliongoza kikao cha kwanza cha kamati hiyo asubuhi ya leo.

Also Read
Uhuru Kenyatta: Afrika imepiga hatua kukabiliana na Malaria

Akizungumza nje ya jumba la Harambee jijini Nairobi akiwa na wanachama wa kamati hiyo, Kinyua alielezea majukumu ya kamati hiyo ambayo ni pamoja na Kuhakikisha ukabidhi wa mamlaka usio na matatizo yotote kati ya Rais anayeondoka na rais mteule.

Also Read
Kenya Airways yarejelea safari za ndege kutoka Nairobi hadi New York

Kamati hiyo is imejukumiwa Kuhakikisha ulinzi wa kutosha kwa rais mteule, mawasiliano mwafaka kati ya Rais mteule na anayeondoka na kuandaa hafla ya kuapishwa kwa kiongozi mpya wa nchi.

Kinyua alisema watakuwa wakifahamisha umma Kila mara watakapokuwa wamefikia katika kutekeleza majukumu yao kupitia kwa vyombo vya habari.

Also Read
Kipchoge ahudhuria mechi ya Psg dhidi ya Lille ugani Parc De Princesss

Haya yanajiri wakati ambapo time huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inaendelea kuhakiki matokeo ya uchaguzi wa urais katika kituo kikuu cha kujumlisha kura za urais katika ukumbi wa Bomas kabla ya kutangaza mshindi.

  

Latest posts

Wabunge wa Kenya wawakwatua Wabunge wa Tanzania mabao 3-1

Dismas Otuke

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi