Kampeni ya urais, Kanye West

Mwanamuziki wa Marekani Kanye West alichapisha video yake ya kwanza ya Kampeni za Urais nchini Marekani jumatatu tarehe 12 mwezi Oktoba mwaka huu. Anaonekana kutiilia maanani safari yake ya kutafuta kuingia Ikulu ya White House.

Kwenye hotuba hiyo Kanye West alizungumzia umuhimu wa imani na maombi kwa nchi ya Amerika. Alikuwa akisoma hotuba yake kutoka kwa kielekezi maarufu kama “teleprompter” na nyuma yake kulikuwa na bendera ya Amerika.

Also Read
Familia ya DMX yatoa taarifa kuhusu hali yake hospitalini

Aliahidi kujenga nchi thabiti na akahimiza wamarekani kuwa na maono kwani Amerika sio tu kielelezo kwa ulimwengu mzima bali pia wanafaa kuwa watumishi na wajizoeshe kuinuana.

“Lazima tufanye mambo kwa imani, tukiwa na ujuzi ambao umehakikishwa kwamba tunafuata malengo yanayofaa na kufanya mambo yanayostahili. Tutajenga nchi thabiti tukijenga familia thabiti.” Alisema Kanye kwenye hiyo Video.

Also Read
Bobby Brown Junior ameaga dunia

Awali alisema lengo lake kuu la kuwania Urais nchini marekani ni kuleta utamaduni wa familia katika nchi hiyo. Kuligana naye familia ndizo hujenga jamii katika nchi.

Kanye West ameweka maombi ya kupata hakimiliki za maneno “God Save America” kwa nia ya kuyatumia kuunda mavazi ya kampeni kama yale ya Rais Donald Trump, “Make America Great Again”.

Also Read
Msamaha wa Rais

Haya yanapoendelea ikumbukwe kwamba wakati fulani mke wa Kanye West, Kim Kardashian West alikiri kwamba mume wake ana matatizo ya hisia mseto yaani “Bipolar Disorder” na alihisi kwamba alikuwa akipitia tatizo hilo akitangaza azma yake ya kuwania Urais wa nchi ya Amerika.

  

Latest posts

Mwelekezi Sir Jacob Otieno Ameaga Dunia

Marion Bosire

Daddy Owen Azindua Albamu Mpya

Marion Bosire

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi