Kampeni za chaguzi ndogo za siku ya Jumanne kusitishwa Jumamosi usiku

Wagombea wa nyadhifa mbali mbali za kuchaguliwa wana muda wa hadi Jumamosi usiku kukamilisha kampeini zao kabla ya kufanywa chaguzi ndogo katika maeneo matano humu nchini.

Tume ya mipaka na uchaguzi nchini-IEBC iliratibu shughuli hiyo kuanza tarehe 15 mwezi Oktoba na kumalizika tarehe 12 mwezi Disemba,saa 48 kabla ya shughuli ya upigaji kura kuanza.

Also Read
Afueni kwa Sonko baada ya Mahakama kusimamisha uchaguzi mdogo wa ugavana Nairobi

Chaguzi hizo zitafanywa kumchagua mbunge mpya wa eneo bunge la Msambweni,wawakilishi wapya wa Wadi za Kahawa Wendani katika kaunti ya Nairobi,Kisumu kaskazini na Lake View kaunti ya Kisumu,Dabaso kaunti ya  Kilifi na Wadi za Wundanyi/Mbale katika kaunti ya Taita Taveta.

Also Read
Mahakama kutoa uamuzi leo kuhusu rufaa saba za kupinga BBI

Tume hiyo imesema vituo vya kupigia na kuwianisha kura vitafukizwa dawa kabla ya shughuli hiyo kuanza siku ya Jumanne.

Afisa mkuu wa uchaguzi wa Mswambweni Yusuf Abubakar alisema kuwa shughuli ya kutoa mafunzo kwa maafisa 450 watakaohudumu kwenye vituo vya kupigia kura itakamilika Jumamosi.

Also Read
Idara ya Uhamiaji yasitisha kwa muda shughuli za utengenezaji paspoti

Alisema shughuli za miezi miwili ya kampeini ziliendeshwa bila vurugu na amewahakikishia wapiga kura 69,003 waliosajiliwa kwamba upigaji kura utafanywa kwa kuzingatia taratibu za wizara ya afya za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi