Kang’ata adai barua aliyomuandikia Rais ilikuwa na nia njema kabisa

Seneta wa Kaunti ya Murang’a Irungu Kang’ata ametetea hatua yake ya kumuandikia barua Rais Uhuru Kenyatta kuhusu uungwaji mkono finyu wa ripoti ya BBI katika eneo la Mlima Kenya.

Akiwahutubia waandishi wa habari katika majengo ya bunge, Kang’ata, ambaye ni Kiranja wa wengi katika Bunge la Seneti, amesema yungali mwanachama halisi wa chama cha Jubilee na kwamba hakushawishika na mrengo wowote wa kisiasa kwenye uamuzi wake wa kumuandikia rais mnamo tarehe 30 mwezi uliopita.

Also Read
Watu 961 zaidi waambukizwa COVID-19 Kenya, 854 wapona huku 10 wakiaga dunia

Amesisitiza kwamba wakazi wa eneo la Mlima Kenya wamehisi kuwa mchakato wa BBI ni mpago wa mrengo mmoja wa Jubilee ilhali wanatarajia ajenda iliyojumuisha viongozi wote chamani.

“Watu wetu wanahisi kwamba BBI ni mpango wa kikundi kimoja tu cha chama cha Jubilee. Mlima Kenya inataka BBI inayoshinikizwa na familia moja ya Jubilee iliyoungana,” akasema.

Also Read
KBL na NTSA zakubaliana kutoa mafunzo kwa madereva wa uchukuzi wa umma

Kang’ata amesema aliyoyaangazia kwenye barua hiyo ni kwa nia njema ili kuhakikisha ufanisi wa serikali kwenye mipango yake.

“Maswala niliyoyagusia yalikuwa yenye nia njema kuhakikisha kwamba serikali inafanikiwa. Lazima tuiunge mkono serikali lakini pia lazima tuiambie ukweli,” akaongeza.

Aidha amekanusha madai kwamba uongozi wa chama cha Jubilee unataka aondolewe kama kiranja wa wengi kwenye Seneti, akisema ni kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Amos Kimunya aliye na nia binafsi ya kutaka kuondolewa kwake.

Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza aliyekuwa kamishna wa polisi Duncan Wachira

Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya alimshutumu Kang’ata kwa kuwasiliana na rais hadharani badala ya kufuata kanuni zilizowekwa kama kiongozi kwenye bunge la seneti.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi