Kang’ata atishia kuishtaki serikali ya kaunti ya Murang’a kwa kusitisha kambi za matibabu

Seneta wa kaunti ya Murang’a Irungu Kang’ata ametishia kuishtaki serikali ya kaunti hiyo iwapo haitafutilia mbali barua tata ya kusimamisha kambi za matibabu za bila malipo.

Kang’ata alisema barua hiyo iliyoandikwa na waziri wa afya katika kaunti hiyo, Joseph Mbai, kufutilia mbali kambi za matibabu za bila malipo katika eneo hilo, haina nia njema. 

Aliupatia utawala huo wa kaunti makataa ya siku 14 kufutilia mbali barua hiyo la sivyo atawasilisha kesi mahakamani na kuitisha fidia.

Afisa wa kaunti aliyeandika barua hiyo anapaswa kuifutilia mbali mara moja, la sivyo nitakwenda mahakamani. Kufikia mwezi ujao nilikuwa nimeandaa kambi mbili za matibabu, moja katika kaunti ndogo ya Kandara na nyingine Mathioya,” alisema Kang’ata.

Seneta huyo alisema barua hiyo ya tarehe 21 mwezi Mei kusimamisha kambi zote za matibabu ya bure kwa misingi ya janga laCovid-19, ilikusudiwa kuhujumu juhudi ambazo amekuwa akifanya za kuandaa matibabu ya bure, husuisa kwa watu masikini.

Kangata alisema kambi za matibabu ambazo huwa bila malipo, zimekuwa na manufaa makubwa kwa wale walio na magonjwa sugu kama vile ki-sukari, damu kwenda kasi mwilini, na pia saratani.

Nimekuwa nikiandaa kambi za matibabu bila malipo tangu nilipokuwa mwanachama wa iliyokuwa baraza la manispaa. Wahisani wamekuwa wakifadhili mpango huo na ni aibu kwa mtu kupiga marufuku zoezi hilo ambalo limewanufaisha wengi,” alifoka Kang’ata.

Kangata aliitaka serikali ya kiatifa na zile za kaunti kutayarisha mpango makhsusi wa matibau ya bure kwa wasiobahatika katika jamii.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Visa 511 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi