Kanisa Katoliki lataka maswala tata katika ripoti ya BBI kusuluhishwa

Kongamano la maaskofu wa kanisa katoliki hapa nchini-KCCB, limetoa wito wa maelewano kuhusu masuala tata kwenye ripoti ya maridhiano,BBI ili kuhakikisha ujumuishi kama inavyopendekezwa kwenye ripoti hiyo.

Maaskofu hao wamesema kukubali maoni tofauti katika mchakato wa marekebisho ya ripoti hiyo, ni muhimu katika kuhakikisha umoja wa wakenya.

Also Read
Raila, Gavana Kingi wafokeana hadharani kuhusu chama cha Pwani

Kwenye taarifa, iliyosomwa katika kanisa la Subukia kaunti ya Nakuru na mwenyekiti wa KCCB aliye pia askofu mkuu wa Kisumu Philip Anyolo, viongozi hao wa kidini walisema kwamba wanasiasa wamekuwa wakitatiza mjadala kuhusu  BBI, na kuwakanganya wapigaji kura katika miezi michache iliyopita.

Also Read
Chama cha FORD-Kenya chatangaza msimamo wa kuunga mkono BBI

Askofu Anyolo aliwahimiza wanasiasa wajadilie suala la BBI kwa umakinifu na kujiepusha na matamshi yanayozua migawanyiko.

Aliwahimiza wanasiasa wasaidie katika kuwahamasisha wapigaji kura kuhusu ripoti hiyo.

Aidha maaskofu hao wa katoliki walisema ripoti ya BBI sharti ikaguliwe na wadau mbali mbali ili kurekebisha vipengele ambavyo havitasaidia katika kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini.

Also Read
Kalonzo Musyoka apinga kubuniwa kwa serikali za kimaeneo

Walipinga miongoni mwa masuala mengine, mapendekezo ya kupanua serikali, kuongezwa kwa mamlaka ya rais, kuongezwa kwa idadi ya wabunge na wajibu wa vyama vya kisiasa katika kuteua makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi