Kanye west aendeleza kazi ya “Donda”

Mwaka mmoja tangu tarehe aliyotangaza Kanye ya kutoa rasmi albamu yake, mashabiki wake wamelazimika kuongeza subira hata baada yake kuashiria kuwa tayari kuitoa kwa umma.

Aliandaa kikao cha kusikiliza albamu yake kwa jina “Donda” ambapo alijaza uwanja mzima wa michezo na mashabiki kabla ya Ijumaa tarehe 23 mwezi Julai mwaka huu wa 2021 ambayo alikuwa ametangaza kama siku rasmi ya kutoa kazi hiyo kwa umma.

Also Read
Mercy Johnson apendeza kwenye hafla ya kuwekwa wakfu kwa mtoto wake

Siku hiyo alichelewa kufika kwenye kikao cha kusikiliza albamu yake na alipofika hakusema lolote ila alionekana tu akizunguka kwenye sehemu ya kati Kati ya uwanja akiwa amevaa mavazi ya rangi nyekundu na kufunika kichwa na uso kwa “stocking”.

Also Read
Filamu kuhusu maisha ya Kanye West kuonyeshwa kwenye Netflix

Baadaye aliomba msamaha kwa mashabiki wake kwa kuchelewesha kazi hiyo na inasemekana tangu wakati huo amesalia katika uwanja wa michezo wa Mercedes Benz ili kukamilisha kazi ya albamu ya Donda.

Also Read
Don Jazzy ataja wanamuziki anajuta kutosajili

Amechapisha picha ambayo inaonyesha chumba ambacho analala ndani ya uwanja huo wa michezo.

Hata kama yeye ni tajiri chumba hicho ni cha hadhi ya kawaida mno asingedhaniwa kulala humo.

Zamu hii hajasema ni lini kazi yake ambayo ameipa jina la marehemu mamake Donda West itatoka rasmi.

  

Latest posts

Betty Bayo Afichua Sura ya Mpenzi Wake

Marion Bosire

Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Marion Bosire

Rick Ross Azungumzia Uhusiano Wake na Hamisa Mobeto

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi