Kasisi Pesa adai kuitishwa pesa na kutishiwa maisha baada ya kukutana na Ruto

Mwanzilishi wa Kanisa la Holy Ghost Coptic, Kasisi John Pesa amedai kuwa maisha yake yamo hatarini baada ya kuandamana na viongozi wengine wa kidini kwenye ibada ya Jumapili nyumbani kwa Naibu Rais William Ruto huko Sugoi.

Kasisi huyo anadai kuwa watu wasiojulikana walivamia kanisa lake huko Kanyakwar, Kaunti ya Kisumu siku ya Jumanne wakishinikiza kupewa mgao wa pesa zilizotoka kwa Ruto na kutishia kumuua iwapo atakaidi.

Also Read
Watu 490 zaidi wapona Covid-19 huku 143 wakiambukizwa virusi hivyo

“Ati toa pesa ambazo Ruto alikupatia, tunataka hizo pesa, nikasema sikupewa pesa,” akaeleza Kasisi huyo.

Ziara hiyo ya Sugoi iliyomzulia utata Mhubiri John Pesa, anayesema kuwa baada ya mkutano huo, watu wasiojulikana wamekuwa wakimtumia jumbe za kutishia kumdhuru.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari katika kanisa lake, Kasisi Pesa amesema anatilia maanani vitisho hivyo na ameripoti na kuandikisha taarifa katika vituo vya polisi vya Kondele na Central akiongeza kuwa ziara hiyo kwenye makazi ya Naibu Rais ilikuwa ya maombi pekee wala hakupewa pesa zozote.

Also Read
Wakenya wataja mwaka 2020 kuwa mgumu zaidi

Kasisi huyo ambaye amekuwa akidhihakiwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukosea na kusema kuwa Mfalme Suleimani ndiye alimuua Goliathi kwenye Biblia anasema alishangazwa na matukio ya hivi punde baada ya ziara hiyo.

Also Read
Zaidi ya miti 500,000 ya kiasili kupandwa katika kaunti nane magharibi mwa nchi

Kasisi Pesa anasema kuwa nia yake ilikuwa kufananisha azma ya Ruto ya kuwania urais na jinsi ambavyo Daudi alimuua Goliathi na akajitetea kutokana na kosa hilo akisema uzee pia ulichangia.

Alisema kuwa kama mtumishi wa Mungu anashirikiana na kila mtu na hatahofia kutii mialiko kama hiyo katika siku za baadaye.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi