Kauli ya Kagwe kuhusu chanjo ya Corona yawaudhi Wakenya

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amekashifiwa na Wakenya kutokana na kauli yake kuhusu uvumbuzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Kwenye ukanda wa video iliyosambazwa mitandaoni, Kagwe alionekana kutilia shaka uwezo wa chanjo hiyo iliyosifiwa na wavumbuzi wake.

Waziri huyo anashikilia kuwa fedha za Wakenya walipa ushuru hazitatumiwa kuagizia chanjo ambazo uwezo na usalama wake wa kiafya haujathibitishwa kikamilifu ulimwenguni.

Also Read
Kenya yanakili visa 244 vipya vya covid-19, watu wawili zaidi waaga dunia

Kupitia mitandao ya kijamii, baadhi ya Wakenya wamemkashifu Waziri Kagwe kwa kile walichokitaja kama kauli isiyokuwa na msingi.

Hata hivyo, Kagwe amejitetea kwa kusema kuwa Wakenya hao hawakuielewa kikamilifu kanda hiyo na kuwa waliichukua nje ya muktadha.

Amekariri kwamba serikali ya Kenya itabaki kulichukulia swala hilo na umakini wa hali ya juu.

Also Read
Chama cha Thirdway Alliance chamtaka Rais Kenyatta kulegeza sheria za kukabiliana na COVID-9

“Tunafaa kusubiri chanjo zitakazothibitishwa na wanasayansi wa kimataifa. Tutabaki kuwa waangalifu,” alisema Kagwe.

Siku chache zilizopita, Kampuni za Marekani, Pfizer na BioNTech, zilitangaza kupatikana kwa chanjo yenye uwezo wa kukinga binadamu kwa zaidi ya asilimia 90 dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Also Read
Watu 437 zaidi waambukizwa Covid-19 humu nchini

Kwa mujibu wa kampuni hizo, chanjo hiyo tayari imefanyiwa majaribio ya mwisho mwisho bila kuonyesha matatizo yoyote ya kiafya.

Wakenya wamemshinikiza Rais Uhuru Kenyatta kuangazia swala hilo kwenye hotuba yake ya mwaka huu kuhusu hali ya taifa ambayo anatarajiwa kuitoa leo kwenye kikao maalum cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi