Kaunti ya kwale yashinda makala ya 94 ya muziki na utamaduni nchini

Kaunti ya Kwale iliibuka mshindi katika makala ya 94 ya mashindano ya kitaifa ya muziki na utamaduni, yaliyoandaliwa katika bustani ya Mama Ngina Waterfront Park Jijini Mombasa.

Kaunti hiyo ilizoa alama 253 huku ikifuatiwa kwa karibu na kaunti ya Kakamega kwa alama 247.

Kwale iliibuka mshindi katika vitengo 56, ikaridhika na nafasi ya pili katika vitengo 34 huku ikishikilia nafasi ya tatu katika vitengo 17 katika mashindano kuhusu nyimbo na utamaduni.

Also Read
Mzozo kati ya wakazi wa Kwale na Tume ya Ardhi nchini kuchelewesha ujenzi wa Bwawa la Mwache

Kaunti hiyo ya Pwani iliwasilisha zaidi ya vikundi 30 vya kitamaduni, vilivyojumuisha wachezaji dansi wa kitamaduni chini ya mwavuli wa ‘Utamaduni Team’.

Mnamo mwaka wa 2019, kaunti hiyo ya Kwale iliibuka ya pili katika mashindano hayo yaliyoandaliwa katika kaunti ya Siaya, huku ikizoa zaidi ya tuzo 40 katika vitengo mbali mbali vilivyojumuisha, muziki, mashairi, usanii na densi.

Also Read
Rais Kenyatta akariri kujitolea kwa serikali kukomesha dhuluma za kijinsia

Akizungumza na wanahabari, waziri wa michezo na utamaduni wa kaunti ya Kwale Ramadhan Bungale, alipongeza timu za kaunti hiyo kwa ufanisi huo na pia kujitolea kwao wakati wa mashindano hayo.

“Kaunti ya Kwale ilishikilia nafasi ya pili wakati wa mashindano ya mwaka 2019, lakini sasa tumeibuka washindi, ishara tosha kaunti hii ina utajiri mkubwa wa muziki na utamaduni,” alisema waziri huyo.

Also Read
EACC kuwahoji maafisa wa KPLC kuhusu kasoro za ununuzi

Bungale aliongeza kuwa, serikali ya kaunti hiyo, itavisaidia vikundi vilivyoshinda kuhakikisha utamaduni wa watu wa kwale unahifadhiwa.

Kwa mujibu wa waziri huyo, mashindano hayo husaidia jamii tofauti kufahamu utamaduni wa jamii zingine na pia husaidia kukuza amani kupitia utangamano.

Kaunti ya Kwale inajivunia aina mbali mbali ya tamaduni kutoka kwa jamii za Duruma, Digo, Makonde, Wazaramo, na Kamba.

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Brown Mauzo Azindua Video ya Kibao “Naoa”

Marion Bosire

Wadau wa Filamu Wahimizwa Kutoa Mawasilisho ya Warsha ya Durban

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi