Kaunti ya Murang’a kuanzisha chama cha wachuuzi cha akiba na mikopo

Serikali ya kaunti ya Murang’a inapania kuanzisha chama cha akiba na mikopo kwa wachuuzi kama njia ya kuinua shughuli za kiuchumi miongoni mwa wachuuzi na wafanyabiashara wadogo.

Chama hicho kwa jina Wachuuzi kinanuia kuwaunganisha wachuuzi na wafanyabiashara wadogo na kuwapa nafasi ya kuweka akiba na kuchukua mikopo ili kukuza biashara zao.

Also Read
Mwana amuua babake na kuuteketeza mwili katika kaunti ya Murang'a

Gavana wa kaunti hiyo Mwangi wa Iria amesema serikali yake imeratibu sheria ili kuwezesha kuanzishwa kwa chama hicho mapema mwaka huu.

Wa Iria ambaye alikuwa akizungumza ofisini mwake amesema usajili wa wanachama umeanza na kufikia sasa wachuuzi na wafanya biashara wadogo 30,000 tayari wamejiandikisha.

“Chama hicho kinalenga zaidi ya wanachama 100,000 kuwawezesha kuweka kiwango cha akiba kinachohitajika ili kuanza kutoa mikopo kwa wanachama kando na huduma nyingine za kifedha kwa ustawi wa kiuchumi,” alisema Wa Iria.

Also Read
Viongozi wa Murang'a kuhudhuria mikutano yote ya kisiasa katika kaunti hiyo

Kwa mujibu wa Wa Iria, wachuuzi na wafanyibiashara wadogo hukosa huduma za mikopo kutoka kwa taasisi kuu za kifedha.

“Chama huki cha akiba na mikopo ni muhimu sana kwa wanabiashara kwani wataweza kuwekeza na kupata mikopo,” aliongeza Wa Iria.

Also Read
Ghasia zashuhudiwa katika mkutano wa Ruto huko Murang’a

Gavana huyo wa Murang’a  alisema kuanzia mwezi Januari,maafisa wa chama cha ushirika wataanza kuwapa mafunzo wanabiashara kuhusu umuhimu wa chama cha akiba na mikopo sawia na kupiga jeki zoezi la kuwaandikisha wanachama.

  

Latest posts

Nabulindo ashinda kesi ya kupinga kuchaguliwa kuwa mbunge wa Matungu

Dismas Otuke

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Ibada ya wafu ya daktari Gakara na wanawe wawili yaandaliwa Nakuru

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi