Kaunti ya Nakuru yakumbwa na mzozo wa Kiafya

Kaunti ya Nakuru inakumbwa na mzozo wa kiafya huku nafasi za kuwalaza wagonjwa kwenye hospitali za sehemu hiyo zikipungua kutokana na ongezeko la visa vya ugonjwa wa Korona.

Kamishna wa kaunti hiyo  Erastus Mbui aliuambia mkutano wa kamati ya kukabiliana  na ugonjwa wa Korona  katika Kaunty hiyo kwamba ongezeko la msambao wa virusi vya Korona, huenda ukaathiri huduma za afya.

Also Read
Millie Odhiambo: Marekebisho ya Kikatiba hayatadhoofisha bunge la Senate

Mbui aliiambia kamati hiyo kwamba wakazi wa kaunti hiyo wanapuuza masharti ya kukabiliana  na msambao wa virusi hivyo na ipo haja ya kuhakikisha wameyazingatia.

Also Read
Watu weusi wamo katika hatari maradufu ya kuambukizwa virusi vya Covid-19

Alisema maafisa wa serikali wanaostahili kuonesha mfano mwema kwa umma pia wanapuuza masharti hayo yaliyowekwa na wizara ya afya.

Gavana wa kaunti hiyo Lee Kinyanjui amesema, baada ya kuwapima wakazi wa sehemu za mashambani za kaunti hiyo ambao awali walidhaniwa kutokuwa na virusi hivyo idadi ya waliopatikana navyo ilikuwa kubwa.

Also Read
Kaunti ya Makueni kupokea shilingi Bilioni 3 kutoka Uholanzi kuboresha huduma za Afya

Alisema serikali ya Kaunti ya Nakuru itashirikiana na serikali kuu kuhakikisha masharti ya kuzuia msambao wa ugonjwa huo yanazingatiwa na wote.

 

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi