Kazi mpya kutoka kwa Ben Pol

Mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo Tanzania Benard Michael Paul Mnyang’anga maarufu kama Ben Pol ana kazi mpya iitwayo “B”. B ni mkusanyiko wa nyimbo nne ambazo zote zinahusu mapenzi na anatumia nyimbo hizo kuonyesha safari yake ya mapenzi.

Kulingana na maelezo kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, Ben Pol anasema nyimbo hizo nne kwenye mkusanyiko “B” ni tamko la mapenzi kwa mapenzi yenyewe na kwamba ni hadithi nne za mapenzi kuhusu mapenzi yenyewe.

Also Read
Nandy na Billnass wameachana

Wimbo wa kwanza unaitwa “Kisebusebu” ambao umetayarishwa na Chatta Boi wa kampuni ya kutayarisha muziki ya Vintage Music Worldwide na amemhusisha mwanamuziki Billnass. Kibao hicho kinazungumza kuhusu hali ya wapenzi wawili kutojua walikosimama na wanakokwenda kama wapenzi.

Kibao cha pili kwa jina “For You” kimetayarishwa na Jaco Beatz ambaye ni mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania. Kwenye kibao hicho mpenzi anaangazia mapenzi yao ya awali, anashukuru kwa nafasi alizopatiwa ili kubadili tabia na anajuta kwa kutojitolea kwenye mapenzi hadi mlango ukafungwa kabisa.

Also Read
Sikudhani ataolewa na mtu aliyetalikiwa, Kanyari kuhusu Betty Bayo

Nambari tatu kwenye kazi hiyo ambayo inaitwa “B” ni kibao kwa jina “Unaita”, ambapo Ben Pol anaimba kuhusu kipindi cha fungate ambapo kila kitu kuhusu mpenzi wako kina maana kubwa na anashangaa utamu wa penzi changa.

Also Read
RMD

Mwisho wa “B” ni kibao “Warira” ambacho kinahusu mpenzi kuvunjwa moyo, mazoea ya mapenzi na kutopatiwa fursa ya pili kwenye uhusiano wa kimapenzi ili kurekebisha mambo.

Mwimbaji huyu ambaye maajuzi ametalikiana na aliyekuwa mke wake Anerlisa Muigai wa Kenya anasema liwe liwalo penzi ni jibu, muziki ni chombo huku akisihi mashabiki wafungue nyoyo zao waimbe naye. Kazi hii inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mitandaoni.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi