KCB Wazidi kutesa ligi kuu ya Vipusa baada ya kuwanyofoa NRB Magereza

Klabu ya KCB iliendeleza matokeo bora katika ligi kuu ya wanawake baada ya kuilaza timu ya Nairobi Prisons seti 3 -0 katika mchuano wa ligi kuu uliosakatwa Ijumaa katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Nahodha wa timu ya taifa Malkia Strikers Mercy Moim alikuwa nyota wa mchezo akichangia ushindi wa seti ya kwanza kwa wanabenki pointi 25-15 katika seti kwanza  na kutwaa seti ya pili 25-21 na 25-15 katika seti ya mwisho .

Also Read
Vipusa wa Kenya wa Voliboli ya Ufukweni wacharazwa seti 2-0 na USA

Kocha wa KCB Japheth  Munala amesema ameridhishwa na mchezo unaozidi kuimarika kila kuchao kwa timu yake.

“Kwa sasa tumekuwa tukifanya vyema  na kufanya mazoezi kwa bidii ,mshikamano wa timu  unazidi kuonekana na natumai tutafuzu kwa mchujo wa ligi kuu”akasema Munala

Also Read
Simiyu arejea kuifunza Kenya

Kocha Munala pia anajivunia wachezaji wake wanane walio kwenye timu ya taifa itakayoshiriki michezo ya Olimpiki mwaka huu .

DCI wakipambana na KDF

Kwenye matokeo mengine ya Ijumaa DCI imetoka nyuma na kusajili ushindi wa seti 3-1 dhidi ya KDF,DCI wakipoteza  seti ya kwanza alama 16-25  kabla ya kugutuka na kunyakua seti zilizofuatia pointi  25-19, 25-15 na  25-22 ,kabla ya KDF kuwagaragaza Nairobi Water seti 3-0 za 25-12,  25-15,25-12.

Also Read
Kenya yajumuishwa kundi gumu dhidi ya Moroko na Misri mashindano ya kombe la Voliboli Afrika
DCI wakichuana na Nairobi Prisons

Ligi hiyo sasa itachukua mapumziko kutoa fursa kwa timu ya taifa Malkia Strikers kujitayarisha kwa michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan.

 

 

  

Latest posts

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi