KCB yawafilisi Gor Mahia na kuwapa kipigo cha 4 ligi kuu FKF

Mabingwa watetzi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia waliendelea kutota baada ya kucharazwa mabao 2 bila jibu na Kenya Commercial Bank katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa Jumapili alasiri katika uwanja wa Kasarani.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia sare tasa KCB walirejea kipindi cha pili na mbinu tofauti huku Dennis Simiyu akipigiwa pasi na kupachika bao la kwanza dakika ya 75, huku kipa Bonface Oluoch kimcheza rafu Victor Omondi na kuwazawidi KCB penati iliyofungwa na Omondi akiongeza la pili kunako dakika ya 85 .

Also Read
Chui waizamisha Bandari na kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu
Also Read
Tanzania waitemea Djibouti 'cheche za moto' CECAFA

Ilikuwa ni mechi ya tano kwa Gor Mahia kupoteza msimu huu na ya pili mtawalia huku wakiteremka hadi nafasi ya 8 ligini kwa pointi 19,alama 16 nyuma ya viongozi Tusker Fc waliosakata mechi nne zaidi.

Also Read
Italia yaanza kwa mbwembwe kipute cha Euro

Katika pambano jingine Kakamega Homeboyz ilipata ushindi wa bao 2-1 ugenini dhidi ya Mathare United inayozidi kurekodi matokeo duni msimu huu.

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi