KDF kujenga vibanda vya kuhifadhi mifugo katika ardhi tata Athi River

Maafisa wa vikosi vya ulinzi wa humu nchini (KDF), wameanza kujenga vibanda vya kuwahifadhi mifugo kabla hawajachinjwa kwenye kiwanda cha kampuni ya Kenya meat commission kilichoko Athi River.

Afisa msimamizi wa kiwanda cha KMC Brigadier James Gathaga, anasema usimamizi wa kiwanda hicho cha kutayarishia nyama, unajenga vibanda katika eneo hilo kwa ajili ya mifugo wengi wanaowasilishwa na wakulima.

Also Read
Itachukua Muda mrefu kabla ya maji kupungua katika maziwa ya bonde la Ufa

Maafisa wa kijeshi kwa kushirikiana na polisi wa kawaida wamepelekwa eneo hilo kujenga vibanda vya kuhifadhi mifugo katika eneo la ekari saba za ardhi ambalo ni sehemu ya ardhi ya ekari 2,900 ambazo wakaazi wa eneo la mpaka kati ya kaunti za Kajiado na Machakos wanadai haki ya kuimiliki.

Also Read
John Lonyangapuo na Samuel Poghisio warushiana cheche za maneno

Wakaazi hao wanadai ardhi hiyo ilitengwa na serikali mwaka 1981 kutoka kwa shamba la kampuni ya ufugaji ya Embakasi, chini ya mradi wa kuzalisha mbuzi na kondoo, ambapo ilikubaliwa kwamba endapo mradi huo utakosa kufaulu, ardhi hiyo itarejeshwa kwa jamii.

Also Read
COVID-19: Watu 349 zaidi waambukizwa huku wagonjwa 6 wakiaga dunia

Wameapa kuendeleza jitihada zao huku wakitumainia kurejeshewa ardhi yao.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi