KDF yaahidi uwazi na kuepukana na ufisadi kwenye mchakato wa usajili wa makurutu

Naibu Mkuu Wa Vikosi vya Ulinzi nchini (KDF), Luteni Jenerali Levi Mghalu, ametoa hakikisho kwa Wakenya kwamba zoezi la kuwasajili makurutu watakaojiunga na vikosi hivyo mwaka litafanyika kwa njia huru na ya haki.

Luteni Jenerali Mghalu amesema KDF imefanya mikakati ili kuepusha visa vya ufisadi na kuhakikisha kwamba zoezi hilo litafanyika kwa uwazi ufaao, kwa mujibu wa Sheria ya KDF ya mwaka wa 2012.

Kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa zoezi hilo katika Makao Makuu ya Idara ya Ulinzi Jijini Nairobi, Mghalu ametoa wito kwa Wakenya kuepukana na matapeli wanaoitisha pesa kwa kudai kuwa na ushawishi katika mchakato huo.

Also Read
Ndege ya jeshi ya wanahewa yaanguka Tsavo mashariki

“Wakenya wanakumbushwa kwamba kutoa hongo au vitendo vyengine vya ufisadi ni kinyume cha sheri. Yeyote atakayepatikana akitoa hongo ili apate nafasi kwenye zoezi hili la usajili atajilaumu mwenyewe. Nia yetu ni kuandaa zoezi la usajili lililo huru na haki,” ameonya Mghalu.

Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea hadi tarehe 19 mwezi huu, ambapo maafisa wakuu wa KDF watasimamia usajili huo katika vituo mbali mbali vya Kaunti Ndogo zote kote nchini.

Also Read
Afisa wa zamani wa KDF afungwa jela kwa kosa la ulaghai

Aidha, hafla ya Jumatatu imeaishiria kutamatika kwa uwasilishaji wa barua za maombi kutoka kwa Wakenya wataalamu wenye lengo la kujaza nafasi za taaluma mbali mbali zilizotangazwa na KDF.

Wataalamu watakaoteuliwa kwa mahojiano watajulishwa kati ya tarehe 18 hadi 25 mwezi huu, huku wale makurutu watakaoteuliwa katika kila Kaunti Ndogo watajua hatma zao mara tu baada ya zoezi la usajili kwenye vituo vyao.

Mghalu amekiri kwamba zoezi la usajili la mwaka jana lilikumbwa na jumla ya visa 106 vya ufisadi, ambapo visa 101 kati ya hivyo vilihusisha raia na vitano vilihusisha maafisa wa vikosi hivyo na wahusika wote walichukuliwa hatua mwafaka za kisheria.

Also Read
Waliopoteza uraia wa Kenya washauriwa kutuma maombi ya kurejeshewa

“Ili kuepukana na hali kama hiyo, KDF inaendelea kuhakikisha kwamba umma unakumbushwa mara kwa mara kuripoti matapeli wanaolenga kuwapora pesa zao,” akasema Mghalu.

Kumekuwa na malalamishi kutoka kwa umma kwamba zoezi la usajili huo halifanyiki kwa njia huru, huku Wakenya wengi wakipoteza maelfu ya pesa kwa watu wanaodai kuwa na uwezo wa kushawishi matokeo ya usajili huo.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi