KDF yawalaza wagonjwa kwa matumaini baada ya kuwazawadi Krismasi

Ilikuwa ni siku kuu njema kwa wagonjwa katika hospitali ya vikosi vya ulinzi ya Defence Forces Memorial, baada ya usimamizi wa hospitali hiyo kuwazawadi na kujumuika nao kusherehekea siku kuu ya Krismasi.

Also Read
Wanaopinga usajili wa Huduma Namba awamu ya pili wakosolewa

Hafla hiyo iliyoongozwa na afisa mkuu wa matibabu wa hospitali hiyo Brigedia Dkt. Charles King’ori,  ilileta tabasamu na afueni kwa wagonjwa hao huku matumaini yao ya kupona yakihuishwa.

Wahudumu wa hospitali hiyo walikata keki pamoja na kuwapa zawadi wagonjwa hao, zikiwemo kadi za kuwatakia afueni ya haraka.

Also Read
Wanariadha watakaoshiriki Kip Keino Classic kubainika Septemba 25

Katika ujumbe wake wa Krismasi kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia ni amiri jeshi mkuu,  aliwakumbusha wakenya kudhihirisha upendo wa yesu Kristo kwa kutoa na kushiriki pamoja na wale wasiojiweza katika jamii.

Also Read
Gazeti moja laagizwa kumlipa Mbunge Mohammed Ali shilingi milioni moja kwa kumchafulia jina

Siku kuu ya Krismasi huadhimishwa na wakristo kila tarehe 25 mwezi Disemba, kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi