KEMSA yaanza kusambaza vyandarua milioni 10 katika kaunti za Pwani

Shirika la Usambazaji wa Bidhaa za Matibabu Nchini (KEMSA)limeingia katika awamu ya tatu ya usambazaji wa vyandarua milioni 10 vilivyopakwa dawa za kuua mbu ili kuimarisha udhibiti wa maradhi ya malaria.

Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo, Edward Njoroge, anasema awamu ya tatu ilianza mwishoni mwa mwezi uliopita na inatarajiwa kukamilika katikati ya mwezi huu.

Wanaolengwa katika awamu hiyo ni watu wasiojiweza katika kaunti za Lamu, Kwale, Mombasa, Kilifi na Tana River.

Alisema chini ya Awamu ya kwanza, shirika hilo lilisambaza vyandarua zaidi ya milioni moja katika kaunti za Kirinyaga, Baringo, Marsabit, Turkana na Vihiga.

Katika awamu ya pili, alisema shirika hilo lilisambaza vyandarua milioni tatu huko Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori.

Awamu ya nne iliyopangwa kuanza mwezi Mei italenga kaunti za Bomet, Nyamira, Kisii, Nandi, Kericho, Uasin Gichu, Taita Taveta, Pokot Magharibi na Trans Nzoia.

Afisa huyo alishukuru Hazina ya Kimataifa, Idara ya Udhibiti wa Malaria na Hazina ya Kitaifa kwa kuchukua jukumu muhimu katika kusaidia kudhibiti maradhi ya malaria humu nchini.

Njoroge alisema ushirikiano na wadau wote muhimu ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kuboresha utoaji wa huduma za afya.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi