KEMSA yasambaza barakoa kwa wanafunzi wasiojimudu nchini

Halmashauri ya usambazaji dawa nchini-KEMSA imeanzisha usambazaji barakoa ambazo zinaweza kutumika tena kwa wanafunzi wa shule za msingi na upili kutoka familia zisizojimudu.

Kwenye taarifa afisa mkuu mtendaji wa halmashauri ya KEMSA, Edward Njoroge, alisema jumla ya barakoa 637,407 zitasambazwa katika eneo na Nairobi na viungani vyake mwezi huu.

Hii ni kutokana na visa vingi vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 ambazo vimeripotiwa katika eneo hilo.

Kaunti ya Nairobi itapokea barakoa 34,641 kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 6, barakoa 57,723 zitatolewa kwa wanafunzi walio na umri wa kati ya miaka 6 na 12 na barakoa 48,641 zitatolewa kwa wanafunzi walio na umri wa miaka 13 na zaidi.

Also Read
Waathiriwa 300 wa mkasa wa moto Kangemi wapata msaada kutoka kwa Ananda Marga Mission

Kaunti ya Murangá itapokea barakoa 39,869 kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 6, barakoa 43,980 kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6 na 12 na barakoa 84,003 kwa wanafunzi walio na umri wa miaka 13 na zaidi.

Also Read
Chama cha ANC chamteua Peter Nabulindo kama mgombea wake kwenye uchaguzi mdogo wa Eneo-Bunge la Matungu

Kaunti ya Kiambu itapokea barakoa 90,600 kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 6, barakoa 60,914 kwa watoto walio na umri wa kati ya miaka 6 na 12 na barakoa 96,469 kwa wanafunzi waliona umri wa miaka 13 na zaidi.

Kaunti ya kajiado itapokea barakoa 50,936 kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 6, barakoa 6,670 kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6 na 12 na barakoa 22,954 kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 13 na zaidi.

Also Read
Tume ya PSC yazawadiwa na KRA kwa ulipaji bora wa ushuru mwaka 2020

Shule ya kwanza iliyonufaika na mpango huo ni ile ya msingi ya Mwiki katika kaunti ya Kiambu ambayo ni mojawapo ya shule zenye idadi kubwa zaidi ya wanafunzi hapa nchini.

Shule hiyo ilipokea barakoa 4,320 za kutolewa kwa wanafunzi 3,991 katika shule hiyo.

Njoroge alisema halmashauri ya KEMSA ina shirikiana kwa karibu na shirika la taifa la biashara kuhakikisha barakoa hizo zinasambazwa kwa wakati ufaao barakoa zilizosalia ambazo zimejumuishwa kwenye mpango huo.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi