Kendrick Lamar Kuandaa Ziara ya Ulimwengu

Baada ya kutoa kikamilifu albamu yake inayofahamika kama “Mr. Morale & The Big Steppers” mwanamuziki wa Marekani Kendrick Lamar ametangaza ziara ya ulimwengu. ziara hiyo ambayo ameipa jina la “The Big Steppers Tour” itaanza mwezi Julai nyumbani Marekani ambapo atazuru sehemu kadhaa na imalizike mwezi Disemba na kulingana na orodha ya maeneo ambayo atazuru, eneo la mwisho kuzuru ni New Zealand. Tangazo hilo aliliweka kwenye Instagram Stories.

Also Read
Roma Zimbabwe azomea wanamuziki wenza

Albamu hiyo ya Lamar ya mwisho chini ya kampuni ya Top Dawg Entertainment imesifiwa kwa kuangazia maswala ya afya ya akili. Kwenye nyimbo hizo, Lamar amezungumza kuhusu maisha yake ambapo alikabiliana na matatizo ya kiakili akatafuta usaidizi na akakaa kwa muda wa miaka miwili bila uwezo wa kuendelea kuandika nyimbo au mashairi almaarufu, “writer’s block”. Kazi hii imejiri miaka mitano baada ya Lamar kuzindua albamu kwa jina “Damn”.

Also Read
J. Cole Arejelea Mchezo wa Mpira wa Kikapu

Alifikia mahali akaomba Mungu amsaidie na anasema Mungu alijibu maombi yake. Kazi yake ya hivi punde ni dhihirisho la maombi yaliyojibiwa kwani albamu ina nyimbo 18 ambazo muda jumla ni zaidi ya dakika 75 na kila wimbo unafurahisha kusikiliza na ni kama hadithi.

Also Read
"Serikali tafadhali mchukulie hatua!" Msizwa

Mwanamuziki huyo amejishindia tuzo kadhaa kutokana na umahiri wake. tuzo zake kwa jumla ni 161 kutokana na uteuzi mara 399. Zinajumuisha 14 za Grammy, sita za Billboard Music Awards na ile ya ASCAP Vanguard Award kutokana na utunzi wake.

  

Latest posts

Kourtney Kardashian na Travis Barker wafunga ndoa kwa mara ya tatu

Tom Mathinji

Wimbo mpya wa Bahati wapata ufuasi wa watu milioni moja

Tom Mathinji

Wizkid asema albamu yake mpya imekamilika

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi