KeNHA yakabili msongamano wa magari unaosababishwa na ujenzi wa barabara ya moja kwa moja Nairobi

Halmashauri ya kitaifa ya usimamizi wa barabara kuu (KeNHA) imesema inashirikiana na maafisa wa polisi kukomesha msongamano wa magari kwenye barabara inayounganisha eneo la Mlolongo na barabara ya James Gichuru jijini Nairobi.

Kwenye taarifa, halmashauri hiyo imesema ujenzi unaoendelea wa barabara kuu ya moja kwa moja ya Nairobi na kuhamishwa kwa mabomba ya maji na nyaya za stima kumeathiri shughuli za usafiri kwenye barabara hiyo.

Also Read
Makanisa ya Nairobi, kaunti zengine 4 yarejelea ibada za mitandaoni

Aidha mvua inayoendelea imetatiza shughuli za kawaida baada ya mitaro iliyochimbwa kando ya barabara ili kuondoa maji kufungana na kusababisha mafuriko.

Also Read
Watu 184 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Halmashauri hiyo imesema imeanzisha juhudi za kuziba mitaro hiyo katika maeneo kadhaa ikiwemo kwenye mzunguko wa uwanja wa taifa wa Nyayo kuhakikisha shughuli za kawaida zinarejelewa kwenye barabara hiyo.

Also Read
Kenya yanakili kiwango cha chini zaidi cha maambukizi ya Covid-19

Kufikia sasa inaweza kumchukua mtu masaa mawili kutoka Mlolongo hadi Westlands wakati wa msongamano lakini mradi huo utakapokamilika, inatarajiwa kwamba utasaidia kupunguza muda huo hadi dakika 20 tu.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi