Kenya imejiandaa vilivyo kukabiliana na aina mpya ya Covid-19

Wizara ya afya imesema iko macho kukabiliana na msambao wa aina mpya ya virusi vya Covid-19.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe akiongoea katika kaunti ya Narok,alipokagua hosipitali ya rufaa ya Narok,alisema serikali haitasita kutangaza hatua zaidi za kuzuia msambao wa virusi hivyo kukiwa na haja ya kufanya hivyo.

Aliwahimiza Wakenya kuendelea kuzingatia kanuni zilizotangazwa na wizara ya afya kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Kenya inatarajia dozi millioni 24 za chanjo ya kampuni ya AstraZeneca mwezi huu ,ambayo imeidhinishwa na shirika la afya duniani ,WHO kwa matumizi ya dharura.

Hayo yamejiri huku nchi hii ikithibitisha visa vipya 174 vya maambukizi ya korona kutoka kwa sampuli 2,848 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa hapa nchini sasa imeongezeka hadi 103,188.

Wagonjwa wawili zaidi pia wameaga kutokana na ugonjwa huo katika saa 24 zilizopita na kuongeza idadi jumla ya vifo hadi 1797.

Idadi ya waliopona kutokana na ugonjwa huo ni watu 85,336 baada ya kudhibitishwa kupona kwa wagonjwa 86 katika muda wa saa 24 zilizopita

Wagonjwa 258 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini huku wengine 1, 190  wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa maambukizi ya visa vipya huku ikinakili visa 124. Mombasa ilifuata kwa visa 9, huku Kiambu ikinakili visa 7.

Kaunti ya kilifi na Uasin Gishu zilinakili visa 4 kila moja huku Murang’a na Machakos zikiwa na visa 3 kila moja.

Kaunti ya Embu na Kajiado ziliandikisha visa 2 kila moja huku Kirinyaga, Makueni,Migori, Taita Taveta,Elgeyo Marakwet na Wajir zikiandikisha kisa kimoja kila kaunti.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi