Kenya inatarajia kupokea shehena ya chanjo ya Johnson and Johnson siku ya Ijumaa hii ikiwa sehemu ya dozi million 4.16 za chanjo ya Covid-19 zitakazopokewa katika muda wa wiki nne zijazo.
Kulingana na katibu mwandamizi wa wizara ya Afya Susan Mochache, ambaye Alhamisi asubuhi alipokea shehena ya chanjo mpya kutoka kwa kaimu balozi wa Canada humu nchini David Anthony Da Silva katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, shehena ya hivi punde itapiga jeki kampeini za chanjo zinazo-endelea kote nchini.
Aliwakumbusha wakenya kwamba chanjo zote zinatolewa bila malipo, huku akiwahimiza waKenya kuwa waangalifu na kutoa habari kwa wizara ya afya kuhusu shughuli zozote haramu za utoaji chanjo kupitia nambari 719 ambayo hailipishwi chocohote.
Dozi nyingine 459,300 za chanjo ya AstraZeneca, ambazo ziliwasilishwa humu nchini kupitia kwa mpango wa Covax, zinafikisha 4,069,900 idadi-jumla ya dozi za chanjo ya Covid-19 ambazo hadi sasa zimetolewa kwa WaKenya.
Jumla ya WaKenya wapatao 806,404 tayari wamepokea chanjo zote mbili za Astrazeneca kote nchini.
Hii inashiri asilimia 2.96 ya idadi jumla ya watu wazima hapa nchini kenya. Alisema WaKenya 1,985,905 wamepokea chanjo ya kwanza.