Kenya kupokea dozi milioni 24 ya chanjo dhidi ya Covid-19

Kenya itapokea shehena ya dozi milioni  24 ya chanjo ya maradhi ya COVID 19 kwa hisani ya mkakati wa COVAX.

Mkurugenzi wa huduma za afya Dkt. Patrick Amoth amesema kuwa shehena hiyo ni ya bila malipo na lakini akasisitiza kuwa taifa hili limeagiza dozi milioni 12 zaidi za chanjo hiyo kwa gharama ya shilingi bilioni kumi.

Also Read
KEMFRI: Samaki wa ziwa Naivasha ni salama

Hata hivyo alisisitiza kuwa ni asilimia 30 ya wakenya ndio watakaopokea chanjo hiyo ya COVID-19 mwanzoni mwa mwaka ujao.

Kwa mujibu wa  Amoth, dozi za kwanza milioni 24 zitakazotolewa kwa hisani ya shirika la COVAX zitashughulikia asilimia  20 ya idadi jumla ya watu kama inavyohitajika na mpango wa shirika la afya ulimwenguni –WHO.

Also Read
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aambukizwa Corona

Dozi milioni 12 zaidi zitakazonunuliwa na serikali zikishughulikia asilimia kumi ya idadi jumla ya watu.

Amoth alisema kuwa wizara ya afya iliwasilisha ombi lake la chanjo hizo tarehe saba mwezi huu.

Also Read
Mwanamke tapeli akamatwa Mombasa kwa wizi wa shilingi milioni 1.7

Shirika la  COVAX lilibuniwa na mashirika ya  GAVI, UNICEF na shirika la afya duniani –WHO ili kutoa chanjo bilioni mbili za dozi za COVID-19 kwa mamilioni ya watu barani  Africa, Asia,  Caribbean na Pacific na barani ulaya kufikia mwisho wa mwaka wa  2021.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi