Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Kenya inatarajia kupokea dola miliona 150 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 16.7, kutoka kwa benki ya dunia katika juhudi za kukabiliana na athari za ukame ambao umeghubika baadhi ya sehemu za hapa nchini.

Hazina kuu imesema kuwa bodi ya wakurugenzi wa benki ya dunia, waliidhinisha fedha hizo ambazo zitatumiwa kupiga jeki juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga nchini Kenya, kupitia mpango wa miaka kumi kuhusu hali ya anga unaoongozwa na serikali na ambao ulizinduliwa mwezi Juni mwaka 2020.

Also Read
Serikali imetwaa ekari 500,000 za ardhi ya misitu katika muda wa mwaka mmoja uliopita

“Mabadiliko ya hali ya anga, yanasalia kuwa changamoto kuu, huku taifa hili likiathirika pakubwa na mafuriko na kiangazi. Tunahitaji kuweka mikakati ya kukufua sekta kama vile Kilimo, Utalii na wanyamapori, maji na kawi ambazo hazikuathiriwa tu na mabadiliko ya hali ya anga, mbali pia na janga la Covid-19,” alisema Ukur Yatani ambaye ni waziri wa fedha.

Also Read
Serikali za kaunti zapokea shilingi bilioni 24.6 kutoka hazina kuu

Mnamo tarehe 8 mwezi Septemba mwaka 2021, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza ukame unaoshuhudiwa hapa nchini kuwa janga la kitaifa huku hazina kuu ikitoa shilingi bilioni mbili za kuwasaidia wanaokumbwa na baa la njaa.

Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza mbunge wa zamani wa kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga

Fedha hizo zilikusudiwa kutabiri, kujiandaa na kukabiliana na athari za hali ya angakatika maeneo husika.
Takriban watu milioni 2.4 wanasemekana kukabiliwa na baa la njaa katika maeneo kame hapa nchini.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi