Kenya Lioness yafuzu kwa mashindano ya FIBA Afrobasket baada ya kuwazabua Misri 99-83

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa kikapu kwa wanawake Lionesses imefuzu kwa mashindano ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kustahimili upinzani mkali na kuwabwaga misri pointi 99-83 kwenye fainali ya mechi za kufuzu Zone 5 iliyochezwa Jumamosi jioni mjini Kigali Rwanda.

Also Read
Harambee Stars yafungua Kambi ya mazoezi kujiandaa kuikabili Misri Alhamisi

Kenya Lionesses walishinda robo  mbili za kwanza pointi  21-18,n1 29-24 huku  na kuongoza  alama 50-42 kufikiwa mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Robo ya tatu ilikuwa ngumu ikimalizikia sare ya alama 27-27 na kisha vipusa wa Kenya wakatwaa robo ya mwisho alama 22-14 na kuwahi tiketi ya kwenda Younde Cameroon kwa mashindano ya Afrika.

Also Read
Lionesses inayoponzwa na majeraha kuvaana na Colombia Jumatano uwanjani Nyayo

Kenya walikuwa wamepoteza kwa pointi 1 dhidi ya Misri katika mechi ya ufunguzi waliposhindwa alama 106-107.

Kuelekea Fainali Kenya ilikuwa imewabandua wenyeji Rwanda alama 79-52 katika nusu fainali siku ya Ijumaa.

 

Rwanda iliridhia nafasi ya tatu baada ya kuwalea Sudan Kusini alama 83-56 na kunyakua nishani ya shaba.

Also Read
Wengine 413 waambukizwa COVID-19 Kenya

Kenya Lionesses sawa na timu ya wanaume zimefuzu kushiriki mashindano ya Afrika kwa mara ya kwanza.

Mashindano ya Afrika yataandaliwa mjini Younde Cameroon baina ya Septemba 17 na 22 mwaka huu.

  

Latest posts

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

NCIC kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani kabla ya msimu wa uchaguzi

Tom Mathinji

Tusker ,Gor Mahia kufungua pazia kwa mechi ya Super Cup Jumatano

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi