Kenya Lionesses kumenyana na Misri fainali ya FIBA Afrobasket Zone 5 Jumamosi

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa kikapu kwa wanawake maarufu kama Kenya Lionesses ,itachuana na Misri Jumamosi jioni , kwenye fainali ya michuano ya FIBA Afrobasket zone 5, kuwania tiketi moja ya kushiriki mashindano ya bara Afrika.

Lionesses waliokuwa wamepoteza mechi mbili za ufunguzi walijizatiti na kuwacharaza wenyeji Rwanda alama 79-52 Ijumaa jioni katika nusu fainali ya pili katika ukumbi wa Kigali

Also Read
Kuahirisha chaguzi za Afrika kwafaa licha ya mizozo ya kikatiba asema Dkt Matsanga

Ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Kenya baada ya kushindwa na Misri na Rwanda katika mechi za awali.

Also Read
Brenda Wairimu avikwa taji ya muigizaji bora Afrika mashariki

Msri ilijikatia tiketi kwa fainali kufuatia ushindi wa pointi 99-65 dhidi ya Sudan Kusini katika semi fainali ya kwanza Ijumaa.

Itakuwa mara ya pili kwa Kenya kukutana na Misri baada ya  Misri kuwalemea vipusa wa Kenya pointi 107-106 katika mchuano wa ufunguzi mapema wiki hii.

Also Read
Michezo yafunguliwa nchini

Fainali ya Jumamosi itang’oa nanga saa tisa alasiri na itatanguliwa ne mechi ya nafasi ya 3 na 4 kati wenyeji Rwanda na Sudan Kusini.

Mshindi wa fainali atafuzu kuwakilisha ukanda huu kwa mashindano ya kombe la Afrika baadae mwaka huu.

  

Latest posts

Chama cha Social Democrats chatwaa ushindi nchini Ujerumani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Ibada ya wafu ya daktari Gakara na wanawe wawili yaandaliwa Nakuru

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi