Kenya Lionesses yaondoka nchini kuelekea Kurume Japan kwa matayarisho ya Olimpiki

Timu ya taifa ya raga ya wanawake 7 upande ilikuwa ya tatu kuondka nchini Jumapili usiku kwenda mjini Kurume Japan kwa matayarisho ya kabla ya kuanza kwa makalaya 32 ya micheoz ya Olimpiki.

Also Read
Mashabiki hawataruhisiwa uwanjani Kasarani mechi ya Kenya na Misri

Lionesses wanavyofahamika watajiunga na wenzao wa kiume pamoja na timu ya voliboli ya wanawake,Malkia strikers katika kambi ya Kurume hadi tarehe 18 mwezi huu,kabla ya kusafiri kwenda Tokyo Julai 19.

Also Read
Raja Casablanca ya Moroko na JS Kabylie kutoka Algeria kushuka Cotonou Benin kuwania kombe la shirikisho


Timu za Shujaa na Malkia strikers zilikuwa za kwanza kuwasili Kurume mapema Jumamosi na Jumapili iliyopita.

Michezo ya Olimpiki itaandaliwa baina ya Julai 23 na Agosti 8 huku Kenya ikiwakilishwa katika fani za riadha,ndondi,uogeleaji,Taekwondo,raga na Voliboli.

Also Read
Elain Thompson awaongoza vidosho wa Jamaica kufagia medali zote za mita 100

Kwa Jumla kenya itatuma ujumbe wa watu 150 katika michezo ya Olimpiki itakayofuatiwa na Olimpiki kwa walemavu.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi