Kenya na Uganda zaafikiana kuondoa vikwazo vya kibiashara

Kenya imeihakikishia Uganda na masoko ya usafirishaji wa bidhaa, huduma bora za kushughulikia bidhaa zinazopitia kwenye bandari zake.

Kwenye taarifa ya pamoja, Kenya na Uganda zimekubaliana kuondoa vikwazo vya kibiashara ambapo bidhaa zilitozwa ushuru kinyume cha kanuni na taratibu za mkataba wa biashara wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Also Read
Afisa wa KDF ashtakiwa kwa kumnajisi msichana wa miaka 16 Nyeri

Ujumbe kutoka Kenya, ukiongozwa na Waziri wa Biashara Betty Maina, ulizuru nchini Uganda kulijadili swala hilo baada ya taifa hilo kulalamikia hatua ya Kenya kutoza ushuru bidhaa zinazoagizwa nchini humo na kupiga marufuku bidhaa za maziwa  na kuku.

Also Read
Kocha Ghost Mulee awataja wasaidizi wake

Maina alikutana na mwenyeji wake wa Uganda Amelia Kyambadde na vile vile Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ambapo pande Zote mbili zilikubaliana kuondoa ushuru huo.

Also Read
Magoha: Asilimia 100 ya wanafunzi wamejiunga na kidato cha kwanza

Nchi hizi mbili zimekubaliana pia kutekeleza kwa ushirikiano shughuli ya kuchunguza ubora wa sukari kutoka nchi hizi mbili na vile vile kujadili changamoto kuhusiana na biashara ya kuku, mahindi, bidhaa za maziwa na bidhaa nyinginezo.

  

Latest posts

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuvuruga amani hapa nchini

Tom Mathinji

Watu wawili wafariki baada ya mashua kuzama Homa Bay

Tom Mathinji

Bunge lachunguza nyongeza ya bei za mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi