Kenya na Zimbabwe zimefungiwa nje ya mechi za kufuzu kwa fainali za kombe la AFCON mwaka ujao nchini Ivory Coast.
Mataifa hayo mawili yalitarajia kuondolewa marufuku ya FIFA wiki mbili zilizopita, ili kuruhusiwa kushiriki mechi za makundi kufuzu kwa kombe la AFCON zitakazoanza mwezi ujao .
FIFA ilipiga marufu Kenya na Zimbabwe kutoka soka ya kimataifa kutokana na mwingilio wa serikali katika usimamizi wa soka.
Hatua hii ina maana kuwa kundi C ambalo litasalia na timu za Cameroon,Burundi na Namibia, baada ya Kenya kuondolewa wakati kundi K, likisalia na Morocco, Afrika Kusini na Liberia baada ya Zimbabwe kuondolewa .