Kenya yaashiria kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19

Kenya imeashiria kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19, huku ikinakili visa vya chini zaidi vya virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Wizara ya afya imetangaza visa 48 vipya vya maambukizi ya Covid-19 katika muda wa saa 24, idadi ambayo imepungua zaidi ikilingaishwa na idadi iliyonakiliwa siku iliyotangulia ya visa 188 katika muda wa kipindi sawia na hicho.

Also Read
Rais Kenyatta: Serikali imejitolea kuboresha mpango wa afya kwa Wote

Visa hivyo vipya 48 vinaongeza idadi jumla ya visa vya maambukizi humu nchini hadi 36,205.

Katika taarifa ya kila siku kuhusu ugonjwa wa Covid-19 humu nchini iliyotolewa Jumatatu, katibu mkuu mwandamizi katika wizara ya afya Dkt Mercy Mwangangi alitangaza kwamba sampuli 1,081 zilipimwa katika kipindi hicho.

Kati ya visa hivyo vipya, 31 ni wa kiume huku 17 wakiwa wa kike huku aliye na umri  mdogo zaidi akiwa na miaka 12 na mkongwe zaidi akiwa na miaka 75.

Also Read
Kenya kwanza yapinga ombi la wizara ya fedha lakutaka mkopo zaidi

Kaunti ya Mombasa iliongoza kwa idadi ya maambukizi huku ikinakili visa 20 ikifuatiwa na Kaunti ya Nairobi kwa visa 15.

Kulingana na katibu huyo mwandamizi wa afya, wagonjwa 176 zaidi wamepona.

Kati ya wagonjwa hao waliopona,45 walikuwa chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani huku wengine 131 wakiruhusiwa kuondoka katika hospitali mbalimbali kote nchini.

Also Read
Rais kenyatta atoa wito kwa wakenya kuendelea kuliombea taifa hili

Idadi jumla ya wagonjwa waliopona humu nchini sasa ni  23,243.

La kusikitisha ni kwamba  wagonjwa wawili zaidi wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha  624  idadi jumla ya wale walioaga dunia humu nchini kutokana na Covid-19.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi