Kenya yaipiga kumbo Sudan na kutinga nusu fainali Cecafa

Timu ya taifa ya Kenya kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20, imefuzu kwa nusu fainali ya michuano ya Cecafa inayoendelea mjini Arusha

Tanzania, baada ya kuilaza Sudan mabao 2-1 katika pambano la mwisho la kundi C uwanjani Sheikh Amri Abeid .

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia kwa sare tasa ,Fortune Omoto aliondoa ukame  wa mabao kwa bao la dakika ya 62 kwa Kenya , lakini zikisalia dakika tano mechi ikatike Ali Gozoli Nooh akavunja nyoyo za wakenya kwa bao kusawazisha .

Also Read
Malkia Striker wapoteza mechi ya tatu mtawalia dhidi ya mabingwa wa dunia Serbia katika Olimpiki

Hata hivyo Benson Ochieng alipachika bao la dakika ya 92  na kuhakisha Kenya maarufu kama rising stars ,wanamaliza kwenye nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 6 kutokana na mechi mbili na kufuzu kwa nusu fainali ya Jumatatu  dhidi ya Hippos kutoka Uganda huku Tanzania walioongoza kundi A wakiweka miadi ya kumenyana na  Sudan kusini katika nusu fainali ya pili pia Jumatatu.

Also Read
Ratiba ya mbio za nyika nchini yakarabatiwa
Nahodha wa Kenya na Sudan wakiwa na waamuzi kabla ya mechi

Timu ya kwanza na ya pili katika michuano hiyo ambayo fainali yake  itapigwa Disemba 2 zitafuzu kushiriki mashindano ya kombe la Afcon kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka ujao nchini Mauritania.

Also Read
Kenya kufungua dimba na Misri Jumatano mashindano ya Voliboli Afrika

Rising Stars walikuwa wamesajili ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya kundi hilo dhidi ya Ethiopia.

 

  

Latest posts

Shujaa kuwinda pointi zaidi Edmonton 7’s

Dismas Otuke

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi